Mon, 09 Mar 2026 | 01:50 PM
Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kimefanya Kikao cha Baraza la Wafanyakazi la NIT Mkoani Morogoro katika ukumbi wa Cate Hotel siku ya Ijumaa tarehe 27 Februari, 2026 ambapo wajumbe ambao ni wafanyakazi wa Chuo wameshiriki.
Akizungumza na wajumbe waliohudhuria kikao hicho Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi NIT Mha. Dkt. Prosper Mgaya amewashukuru wajumbe kwa kushiriki kikamilifu katika kikao hicho kwa kutoa michango katika ajenda mbalimbali zenye mikakati ya kufanya Chuo kuwa kitovu cha ubora zilizowasilishwa na kujadiliwa. Pia, Dkt.Mgaya amewashukuru wasaidizi wake Bi.Husna John (Katibu Baraza la Wafanyakazi NIT) na Bw.Daniel Haule (Katibu Msaidizi Baraza la Wafanyakazi NIT) kwa maandalizi mazuri ya kikao hicho.
Naye Katibu wa RAAWU Kanda ya Mashariki Bw.Meky Humbo amempongeza Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Chuo kwa kuendesha kikao hicho kwa ueledi na hatimaye kuwa chenye mafanikio makubwa.