Fri, 01 May 2026 | 09:48 AM
Naibu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala - NIT, Dkt. Dkt.Zainabu Mshana amefunga rasmi mafunzo ya VIP yaliyoandaliwa kwaajili madereva wanaoendesha viongozi wa jeshi la polisi tarehe 30 Aprili 2026.
Akizungumza na madereva waliohudhuria mafunzo hayo kutoka jeshi la polisi wakati wa hafla ya kufunga mafunzo hayo iliyofanyika katika ukumbi wa Auditorium uliyopo katika kampasi ya Chuo Mabibo Jijini Dar es salaam Dkt. Mshana amelishukuru Jeshi la Polisi kwa kuchagua NIT kama sehemu sahihi kwa madereva hao kupatiwa mafunzo ya VIP daraja la pili.
"Kwa niaba ya Uongozi wa Chuo natoa shukrani za dhati kwa Uongozi wa Jeshi la Polisi nchini kwa kuleta madereva hawa NIT kupata mafunzo haya ambayo ni muhimu kwaajili kuhakikisha viongozi wetu wanakuwa salama"
Aidha, Dkt.Mshana ametoa wito kwa madereva walioshiriki mafunzo hayo kuzingatia yote waliyofundishwa kwa kuzingatia maadili ya kazi na sheria za usalama barabarani.
"Ni matumaini yangu baada ya kuhitimu mafunzo haya mtakuwa mabalozi wazuri kwa kutekeleza majukumu yenu kwa weledi na kuzingatia sheria za usalama barabarani.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Maafisa wa Jeshi la Polisi SCP.Deus Sokoni ameushukuru Uongozi wa Chuo pamoja na wakufunzi wa Chuo kwa kuandaa mafunzo ya VIP kwa madereva wa Jeshi la Polisi.
Mafunzo ya VIP daraja la pili kwa madereva wanaoendesha viongozi wa Jeshi la Polisi yalianza tarehe 1 hadi 30 Aprili 2026 ambapo jumla ya madereva hamsini (50) kutoka Jeshi la Polisi wamehudhuria na kutunukiwa vyeti.