Fri, 18 Jul 2025 | 02:16 PM
Mkuu wa Chuo Dkt. Prosper Mgaya amefungua semina elekezi ya siku mbili (2) ya Viongozi wateule wa Serikali ya Wanafunzi,Students’ Organisation of National Institute of Transport (SONIT) leo tarehe 17 Julai, 2025.
Akizungumza wakati wa ufunguzi Dkt. Mgaya amewaasa viongozi hao kutilia maanani mafunzo hayo kwani ni akiba yao ya siku zijazo ``Viongozi wengi wakubwa walianzia kwenye ngazi ya Chuo au Shuleni hivyo mafunzo ya namna hii siyo ya kuyapuuzia hata kidogo kwani yanaweza kuwasaidia siku zijazo endapo hayatakusaidia kwa sasa``. Amesema
Semina hiyo iliyoandaliwa na Kurugenzi ya Huduma za Wanafunzi ya Chuo imeandaa mada mbalimbali zikiwemo za kupambana na Rushwa ,kufahamu maadili ya kiuongozi na mada zinazohusiana na masuala ya Afya ya akili.
Akizungumzia sababu ya kuandaa mada hizo Mkurugenzi wa Huduma za wanafunzi Ndg. Abel Luzibila amesema kutokana na mabadiliko ya mara kwa mara katika Ulimwengu wa sasa ni vizuri Viongozi kujua juu ya mambo mbalimbali kuhusiana na afya ya akili kwani ni changamoto inalojitokeza sana kwa vijana walio vyuoni .
Ndg. Luzibila amesema tumewaalika watoa mada kutoka Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa, Chuo kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi na Wakufunzi wa hapa kwetu ili kuhakikisha mada zinazotolewa zinatolewa kwa weledi wa hali ya juu.