Fri, 18 Jul 2025 | 02:20 PM
Tarehe 16 Julai 2025, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elim una mafunzo ya Amali Zanzibar Bw. Khalid Masoud Wazir alitembelea banda la Chuo cha Taifa cha usafirishaji (NIT) katika Maonesho ya sita ya Wiki ya Elimu ya Juu yanayoendelea katiika viwanja vya Mnazi Mmoja, Unguja -Zanzibar.
Katika ziara hiyo Bw. Wazir ameipongeza NIT kwa kazi nzuri inayofanya katika utoaji mafunzo, ushauri wa kitaalamu na utafiti. Aidha, amehimiza kuendelea kutoa ushauri wa kitaalamu na kuelimisha wanafunzi kuhusu namna ya kuchagua kozi sahihi kwa maendeleo yao ya kitaaluma, kulingana na ufaulu wao.
Kwa niaba ya Mkuu wa Chuo cha NIT, Dkt. Prosper Mgaya, Kaimu Mkurugenzi Huduma Saidizi Taaluma Bi.Adela Muhale alimshukuru Naibu Katibu kwa kutembelea banda na akaahidi Chuo kuendelea kushirikiana na Serikali ili kuhakikisha malengo ya elimu yanafakiwa kwa ufanisi.
Maonesho ya 6 ya Wiki ya Elimu ya Juu yanaendelea viwanja vya Mnazi Mmoja- Zanzibarkuanzia tarehe 14-20 Julai 2025