Mon, 09 Mar 2026 | 01:51 PM
huo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kimefanikiwa kukamilisha rasmi programu yake ya uhamasishaji (outreach program) ya siku tano (5) iliyofanyika Mkoani Dodoma kuanzia tarehe 23 hadi 27 Februari 2026 ikilenga kutoa elimu na kuwahamasisha wanafunzi wa shule za sekondari kuhusu fursa za masomo ya sayansi na kozi zinazotolewa na Chuo.
Programu hiyo ilifikia jumla ya shule tisa (9) za sekondari zilizopo jijini Dodoma ikiwemo Chinangali,Mkonze,Bunge,Hazina,Mbabala,Nzuguni, Dkt. Samia, Bihawana na Wella.
Katika ziara hiyo, timu ya NIT ilipata nafasi ya kuzungumza na wanafunzi, kuwapa mwanga kuhusu kozi mbalimbali zinazotolewa na Chuo, sifa za kujiunga, pamoja na fursa za ajira katika sekta ya uchukuzi na usafirishaji. Wanafunzi pia walipata nafasi ya kuuliza maswali na kupata ufafanuzi wa kina kuhusu namna ya kutimiza ndoto zao za kitaaluma NIT.