National Institute of Transport - NIT

LATEST NEWS

Wed, 18 Jun 2025 | 01:25 PM

VIONGOZI SERIKALI YA WANAFUNZI WAAPISHWA

National Institute of Transport - NIT

Chuo cha Taifa cha Usafirishaji kimewaapisha viongozi wapya wa Serikali ya Wanafunzi Students` Organization National Institute of Transport (SONIT) kwenye hafla fupi ya uapisho ilifanyika Jumanne tarehe 17 mwezi huu katika viwanja vya NIT Mabibo Campus.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Chuo Dkt. Prosper Mgaya ameipongeza Serikali iliyomaliza muda wake kwa kuwa kiunganishi kizuri baina ya Uongozi wa Chuo na Wanafunzi na hivyo kupelekea kurahisisha utendaji kazi na kusaidia Wanafunzi kusoma kwa amani na utulivu.

Aidha Dkt. Mgaya ameipongeza kurugenzi ya huduma za wanafunzi  ya NIT kwa kuwasimamia vizuri wanafunzi hao katika mambo mbalimbali wanapokua hapa Chuoni. ``Ninyi ndio mko na hawa wanafunzi mara nyingi na kwa kuwa wameonesha nidhamu ya hali ya juu katika maisha yao hapa Chuoni sina budi kuwapongeza sana kwa kuwasimamia vema``. Amesema

Kwa upande wake Rais wa Serikali ya Wanafunzi iliyomai za muda wake Bw. Stavius Alkad amesema katika kipindi cha uongozi wake alipata ushirikiano mkubwa kutoka kwa Uongozi wa Chuo na kwamba amejifunza mambo mengi ya kiuongozi na kuwasihi viongozi wanaongia madarakani kushirikiana vizuri na Uongozi wa Chuo ili wachote busara alizopata yeye

Katika hatua nyingine Dkt. Mgaya amezindua viti vya zege vya kusomea Wanafunzi maarufu kama ``Vimbweta`` vilivyojengwa na Serikali ya SONIT iliyomaliza muda wake, viti hivyo vya kisasa vitawawezesh wanafunzi kusoma hata nyakati za usiku kwani vimefunikwa kwa paa na kuwekwa umeme. Hii ni hatua kubwa sana ambayo Serikali iliyopita imeionesh kama mfano, ni matumaini yangu kuwa Serikali tulioiapisha hivi leo itafanya mambo mengine mkubwa zaidi ukizingatia Rais wa sasa alikua ni Waziri Mkuu katika Serikali iliyopita.

Katika hafla hiyo iliyojaa shamrashamra na maatumaini makubwa kwa wanafunzi juu ya Uongozi mpya ulioapishwa, Mkufunzi wa michezo wa Chuo Bw. Augustino Saquare alikabidhi makombe mawili ambayo timu za wanafunzi zilishinda katika Mashindano ya SHMIVUTA na yale ya SEPESHA RUSHWA yaliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana na timu hizo kuibuka kidedea katika nafasi mbalimbali.

Latest News

National Institute of Transport - NIT

ππˆπ“β€™π’ π…πˆπ‘π’π“ 𝐁𝐀𝐓𝐂𝐇 πŽπ… 𝐉𝐀𝐏𝐀𝐍𝐄𝐒𝐄 π’π‡πŽπ‘π“ π‚πŽπ”π‘π’π„ 𝐑𝐄𝐀𝐂𝐇𝐄𝐒 πŒπ€π‰πŽπ‘ πŒπˆπ‹π„π’π“πŽππ„

May 1, 2026, 9:50 a.m.

The National Institute of Transport (NIT), in collaboration with the Japan International Cooperation Agency (JICA) and the Organization for Technical Enhancement and Industrial Development (OTIDE), marked a significant milestone on 30th April 2026, as the first batch of students in its Japanese short course completed their training, with the ceremony held at the NIT Mabibo Campus.

Speaking during the graduation ceremony, NIT Rector Dr. Prosper Mgaya congratulated the students for their dedication and hard work. He encouraged them to continue strengthening their Japanese language skills and to apply them effectively in their future careers. He also noted the institute’s continued progress in aviation training, proudly highlighting that some graduates are already employed by airline companies as cabin crew. This course will also be a great advantage for aspiring cabin crew, as it equips them with the skills to interact confidently with diverse people, which is essential when applying and advancing in their future careers in aviation.

“We are immensely proud of this milestone you have achieved,” he said. “It reflects not only your academic success, but also your resilience, discipline, and unwavering commitment to personal growth.”

Representing OTIDE, Mr. Godwin Mbaga emphasized the importance of discipline and consistent practice in mastering a new language. He noted that strong language proficiency can create wide-ranging career opportunities for students.

“On her part, Ms. Minako Yamamoto, Senior Representative of JICA, commended the graduates for their commitment and resilience. She underscored the growing partnership between Japan and Tanzania and encouraged them to continue improving their Japanese language skills in order to maximize future opportunities.”

“Completing this course was not easy, especially with your busy schedules,” she said. “I am impressed that you were able to finish. It is not only what you achieve that matters, but how you achieve please stay committed.”

National Institute of Transport - NIT

πŒπ€π…π”ππ™πŽ π˜π€ π•πˆπ πŠπ–π€ πŒπ€πƒπ„π‘π„π•π€ 𝐖𝐀 π‰π„π’π‡πˆ 𝐋𝐀 ππŽπ‹πˆπ’πˆ π˜π€π…π”ππ†π–π€ π‘π€π’πŒπˆ

May 1, 2026, 9:48 a.m.

Naibu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala - NIT, Dkt. Dkt.Zainabu Mshana amefunga rasmi mafunzo ya VIP yaliyoandaliwa kwaajili madereva wanaoendesha viongozi wa jeshi la polisi tarehe 30 Aprili 2026.

Akizungumza na madereva waliohudhuria mafunzo hayo kutoka jeshi la polisi wakati wa hafla ya kufunga mafunzo hayo iliyofanyika katika ukumbi wa Auditorium uliyopo katika kampasi ya Chuo Mabibo Jijini Dar es salaam Dkt. Mshana amelishukuru Jeshi la Polisi kwa kuchagua NIT kama sehemu sahihi kwa madereva hao kupatiwa mafunzo ya VIP daraja la pili.

"Kwa niaba ya Uongozi wa Chuo natoa shukrani za dhati kwa Uongozi wa Jeshi la Polisi nchini kwa kuleta madereva hawa NIT kupata mafunzo haya ambayo ni muhimu kwaajili kuhakikisha viongozi wetu wanakuwa salama"

Aidha, Dkt.Mshana ametoa wito kwa madereva walioshiriki mafunzo hayo kuzingatia yote waliyofundishwa kwa kuzingatia maadili ya kazi na sheria za usalama barabarani.

"Ni matumaini yangu baada ya kuhitimu mafunzo haya mtakuwa mabalozi wazuri kwa kutekeleza majukumu yenu kwa weledi na kuzingatia sheria za usalama barabarani.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Maafisa wa Jeshi la Polisi SCP.Deus Sokoni ameushukuru Uongozi wa Chuo pamoja na wakufunzi wa Chuo kwa kuandaa mafunzo ya VIP kwa madereva wa Jeshi la Polisi.

Mafunzo ya VIP daraja la pili kwa madereva wanaoendesha viongozi wa Jeshi la Polisi yalianza tarehe 1 hadi 30 Aprili 2026 ambapo jumla ya madereva hamsini (50) kutoka Jeshi la Polisi wamehudhuria na kutunukiwa vyeti.

National Institute of Transport - NIT

π–π€π…π€ππ˜π€πŠπ€π™πˆ ππŽπ‘π€ 𝐍𝐀 π‡πŽπƒπ€π‘πˆ ππˆπ“ πŒπ–π€πŠπ€ 𝐖𝐀 𝐅𝐄𝐃𝐇𝐀 πŸπŸŽπŸπŸ“/πŸπŸŽπŸπŸ” π–π€πŠπ€ππˆπƒπ‡πˆπ–π€ π™π€π–π€πƒπˆ

May 1, 2026, 9:47 a.m.

Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mha.Dkt. Prosper Mgaya amekabidhi zawadi mbalimbali kwa wafanyakazi bora na hodari wa Chuo kwa mwaka wa fedha 2025/2026. Watumishi hao wamekabidhiwa zawadi zao ikiwemo fedha taslimu na vyeti tarehe 30 Aprili 2026.

Akizungumza na watumishi wa Chuo wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi kwa wafanyakazi bora na hodari iliyofanyika katika ukumbi wa MPH uliyopo katika kampasi ya Chuo Mabibo Jijini Dar es salaam Dkt. Mgaya amewapongeza wafanyakazi kazi hao kwa kuibuka washindi katika zoezi la kuchagua wafanyakazi bora na hodari wa Chuo lililofanyika hivi karibuni baada ya kuidhinishwa kwa Mwongozo wa Jinsi ya Kumpata Mfanyakazi Bora na Mfanyakazi Hodari wa Chuo.

"Kwa niaba ya Uongozi wa Chuo nawapongeza watumishi wote waliochaguliwa kuwa wafanyakazi bora na hodari katika mwaka huu wa fedha,huu ni mwanzo mzuri natumaini mtakiwakilisha vizuri Chuo katika zoezi la utoaji wa tuzo wakati wa Maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani kitaifa"

Aidha, Dkt.Mgaya amewahakikishia watumishi wa Chuo kuwa zoezi la kutoa motisha mbalimbali kwa wafanyakazi bora na hodari wa Chuo kuwa endelevu na kuboreshwa zaidi.

"Huu ni mwanzo tuu, tutaendelea na utaratibu huu mwakani na kufanya maboresho mbalimbali"

Zoezi la kuchagua wafanyakazi bora na hodari wa Chuo limehitimishwa leo kwa washindi kutangazwa na kukabidhiwa zawadi zao ambapo Mha.Castor Njako ameibuka mfanyakazi hodari wa Chuo, Bi.Rehema Mzee (mfanyakazi bora kada ya wanataaluma),Bw.Meshack Kimaro(mfanyakazi bora kada ya waendeshaji),na wafanyakazi bora katika kundi la ushindani akiwemo Bw.Honest Mrosso, aBw.Robert Kilamato,Bw.Michael Soka,Bw.Juma Msemwa, na CPA.Innocent Mshanga.