Fri, 18 Jul 2025 | 02:18 PM
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Lela Mohamed Mussa, ametembelea banda la NIT katika Maonesho ya 6 ya Wiki ya Elimu ya Juu katika Kilele cha maonesho hayo leo tarehe 17.7.2025 kama Mgeni Rasmi Mnazi Mmoja, Zanzibar.
Akizungumza katika ziara hiyo, Mhe. Lela amesisitiza umuhimu wa kuunganisha elimu ya kitaaluma na mafunzo ya vitendo, akisema Serikali itaendelea kuwekeza katika taasisi kama NIT ambayo inalenga kutoa ujuzi unaokidhi mahitaji ya soko la kazi.
Amesisitiza kuwa elimu si tu maarifa ya kitabiri bali inapaswa kuwa lango la kutoa ajira na kukuza ubunifu nchini.
Kwa niaba ya Mkuu wa Chuo cha NIT, Dkt. Prosper Mgaya, Kaimu Mkurugenzi Huduma Saidizi Taaluma Bi.Adela Muhale alimueleza Mhe. Waziri kuhusu programu mbalimbali za Mafunzo zinazotolewa Chuoni. Waziri alipongeza Chuo kwa mafanikio yaliyopo na kuhimiza Chuo kuendelea na ubunifu katika elimu ya vitendo.
Maonesho ya Wiki ya Elimu ya Juu ya mwaka huu yanakusudia kukuza ushirikiano kati ya vyuo vikuu, taasisi za ufundi na sekta binafsi ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata ujuzi unaohitajika kutimiza ajira.
Maonesho ya 6 ya Wiki ya Elimu ya Juu yanaendelea viwanja vya Mnazi Mmoja- Zanzibarkuanzia tarehe 14-20 Julai 2025