NIT YATOA MAFUNZO YA UKAGUZIWA USALAMAWA BARABARA, MAAFISA USAFIRISHAJI, MADEREVA WAKUU KANDA YA ZANZIBAR

Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kimetoa mafunzo ya Ukaguzi wa Usalama wa Barabara (road safety audit), MaafisaUsafirishaji na Madereva Wakuu. Mafunzo haya ya siku tano yametolewa katika ukumbi wa Chuo cha Mwalimu Nyerere Memorial Academy kampasi ya Zanzibar kuanzia tarehe 22 Januari, 2024 hadi tarehe 26 Januari, 2024 ambapo jumla ya washiriki 253 walihudhuria mafunzo hayo na kutunukiwa vyeti. Akizungumza na washiriki wakati wa hafla ya ufunguzi wa mafunzo hayo, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja ambaye pia alikuwa mgeni rasmi, Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud ameipongeza NIT kwa hatua ya kuandaa mafunzo hayo ili kuwajengea uwezo wataalamu mbalimbali kutoka Zanzibar wakiwemo Maafisa Usafirishaji, Madereva, Wahandisi na Wadau wengine wa usalama barabarani.

DOWNLOAD PDF FILE NIT YATOA MAFUNZO YA UKAGUZIWA USALAMAWA BARABARA, MAAFISA USAFIRISHAJI, MADEREVA WAKUU KANDA YA ZANZIBAR