ORODHA YA WANAFUNZI WALIOPATA NAFASI YA KUISHI HOSTEL ZA NDANI YA CHUO

ORODHA YA WANAFUNZI WALIOPATA NAFASI YA KUISHI HOSTEL ZA NDANI YA CHUO

Hi ni kuwajulisha kwamba, ifuatayo ni orodha ya Wanafunzi waliopata nafasi ya kuishi kwenye hostel za ndani ya Chuo mara baada ya kuwasilisha maombi yao na mchakato wa kuchaguliwa kukamilika.

Aidha, Wanafunzi waliopata nafasi kwenye hostelza Chuo wanapaswa kusoma na kuzingatia maelekezo haya muhimu kama ifuatavyo:-

  • Malipo ya hosteli yanatakiwa kufanyika ndani ya wiki ya kwanza ya usajili yaani tarehe 23/10/2023 m a k a tarehe 29/10/2023 kwa Wanafunzi wote. Aidha, malipo hayo yatafanyika baada ya kupatiwa “Control Number” kutoka katika ofisi za uhasibu hapa chuoni. (Hakikisha kwanza unapata “Control Number” kabla ya kufanya malipo).
  • Mara baada ya kupangiwa chumba/kitanda ni marufuku Mwanafunzi kuhama chumba au kubadilishana kitanda;
  • Endapo itabainika kwamba kumefanyika uharibifu wowote k w e n e chumba Wanafunzi wote wanaoishi katika chumba hicho watachukuliwa hatua za
    kinidhamu;
  • Mwanafunzi yeyote ambaye jina lake limeonekana haruhusiwi kubadilishana nafasi na mwanafunzi mwenzake;
  • Mwanafunzi atakayechelewa kuripoti chuoni baada ya wiki ya kwanza ya usajili kukamilika nafasi yake itachukuliwa na mtu mwingine mwenye uhitaji kwani atakuwa hana sifa tena.