March 9, 2026, 1:52 p.m.
Wanawake wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wameshiriki kikamilifu katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Viwanja vya Barafu Mburahati, jijini Dar es Salaam tarehe 8 Machi 2026.
Maadhimisho hayo yamebebwa na kauli mbiu inayosema;
“Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana: Msingi Jumuishi kufikia Dira 2050.”
Ushiriki huu unaonesha dhamira ya NIT katika kuendeleza usawa wa kijinsia, kuwainua wanawake na wasichana, na kuhamasisha nafasi sawa katika elimu, uongozi na maendeleo ya taifa.
Kwa pamoja tunaendelea kujenga jamii yenye haki, usawa na fursa kwa wote.
March 9, 2026, 1:51 p.m.
huo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kimefanikiwa kukamilisha rasmi programu yake ya uhamasishaji (outreach program) ya siku tano (5) iliyofanyika Mkoani Dodoma kuanzia tarehe 23 hadi 27 Februari 2026 ikilenga kutoa elimu na kuwahamasisha wanafunzi wa shule za sekondari kuhusu fursa za masomo ya sayansi na kozi zinazotolewa na Chuo.
Programu hiyo ilifikia jumla ya shule tisa (9) za sekondari zilizopo jijini Dodoma ikiwemo Chinangali,Mkonze,Bunge,Hazina,Mbabala,Nzuguni, Dkt. Samia, Bihawana na Wella.
Katika ziara hiyo, timu ya NIT ilipata nafasi ya kuzungumza na wanafunzi, kuwapa mwanga kuhusu kozi mbalimbali zinazotolewa na Chuo, sifa za kujiunga, pamoja na fursa za ajira katika sekta ya uchukuzi na usafirishaji. Wanafunzi pia walipata nafasi ya kuuliza maswali na kupata ufafanuzi wa kina kuhusu namna ya kutimiza ndoto zao za kitaaluma NIT.
March 9, 2026, 1:50 p.m.
Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kimefanya Kikao cha Baraza la Wafanyakazi la NIT Mkoani Morogoro katika ukumbi wa Cate Hotel siku ya Ijumaa tarehe 27 Februari, 2026 ambapo wajumbe ambao ni wafanyakazi wa Chuo wameshiriki.
Akizungumza na wajumbe waliohudhuria kikao hicho Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi NIT Mha. Dkt. Prosper Mgaya amewashukuru wajumbe kwa kushiriki kikamilifu katika kikao hicho kwa kutoa michango katika ajenda mbalimbali zenye mikakati ya kufanya Chuo kuwa kitovu cha ubora zilizowasilishwa na kujadiliwa. Pia, Dkt.Mgaya amewashukuru wasaidizi wake Bi.Husna John (Katibu Baraza la Wafanyakazi NIT) na Bw.Daniel Haule (Katibu Msaidizi Baraza la Wafanyakazi NIT) kwa maandalizi mazuri ya kikao hicho.
Naye Katibu wa RAAWU Kanda ya Mashariki Bw.Meky Humbo amempongeza Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Chuo kwa kuendesha kikao hicho kwa ueledi na hatimaye kuwa chenye mafanikio makubwa.
March 3, 2026, 2:37 p.m.
Feb. 17, 2026, 11:32 a.m.
Feb. 17, 2026, 11:32 a.m.
Feb. 17, 2026, 11:31 a.m.
Feb. 13, 2026, 5:02 p.m.
Jan. 21, 2026, 1 p.m.
Nov. 18, 2025, 5:14 p.m.